< ישעה 59 >

הן לא קצרה יד יהוה מהושיע ולא כבדה אזנו משמוע 1
Tazama, mkono wa Yahwe sio mfupi ambao hautweza kukuokoa wewe; wala sikio lake sio zito, ambalo haliwezi kusikia.
כי אם עונתיכם היו מבדלים בינכם לבין אלהיכם וחטאותיכם הסתירו פנים מכם--משמוע 2
Matendo yako ya dhambi, hata hivyo, zimekutenga wewe na Mungu, na dhambi zenu zimemfanya aufiche uso wake msimuone wala kumsikia yeye.
כי כפיכם נגאלו בדם ואצבעותיכם בעון שפתותיכם דברו שקר--לשונכם עולה תהגה 3
Maana mikono yenu ina madoa ya damu na vidole vyenu vimejaa dhambi. Midomo yenu inazungumza uongo na ulimi wenu unazungumza kwa nia mbaya.
אין קרא בצדק ואין נשפט באמונה בטוח על תהו ודבר שוא הרו עמל והוליד און 4
Hakuna hata mmoja aitae haki, na hakuna anayewasihi kesi yake katika haki. Wanayamini maneno yasiyo ya haki, maneno ya uongo; wanashika matatizo na kuzaa dhambi.
ביצי צפעוני בקעו וקורי עכביש יארגו האכל מביציהם ימות והזורה תבקע אפעה 5
Wanetotoa mayai ya nyoka wenye sumu na hufuma mtandao wa buibui. Yeyote alaye mayai yake atakufa, na ikiwa yai litavunjika, litatotoa nyoka mwenye sumu.
קוריהם לא יהיו לבגד ולא יתכסו במעשיהם מעשיהם מעשי און ופעל חמס בכפיהם 6
Mitando yao haitatumika kama mavazi, wala hawawezi kujifukia wenyewe kwa kazi yao. Kazi zao ni kazi za dhambi, na matendo ya vurugu yako mikononi mwao.
רגליהם לרע ירצו וימהרו לשפך דם נקי מחשבותיהם מחשבות און--שד ושבר במסלותם 7
Miguu yao inakimbilia uovu, na wanakimbilia kumwaga damu isiyo na hatia. Mawazo yao ni mawazo ya dhambi; vurugu na uharibifu ndio njia yao.
דרך שלום לא ידעו ואין משפט במעגלותם נתיבותיהם עקשו להם--כל דרך בה לא ידע שלום 8
Njia ya amani hawaijuyui, na hakuna haki katika njia zao. Wametengeneza njia njia zlizopotoka; yeyote atakaye safiri kupitia njia hizi njia hizi hazijui amani.
על כן רחק משפט ממנו ולא תשיגנו צדקה נקוה לאור והנה חשך לנגהות באפלות נהלך 9
Hivyo basi haki iko mbali a sisi, wala haki haijatufikia sisi. Tunasubiri mwanga tunaona giza; tunatafuta mwangaza, lakini tunatembea gizani. Tunapapasa kwenywe ukuta kama kipofu, kama wale wasiona,
נגששה כעורים קיר וכאין עינים נגששה כשלנו בצהרים כנשף באשמנים כמתים 10
Tuna mashaka mchana kweupe kama kwenye mwanga unaofifia; miongoni mwa wenye nguvu tuko kama watu waliokufa.
נהמה כדבים כלנו וכיונים הגה נהגה נקוה למשפט ואין לישועה רחקה ממנו 11
Sisi tunaunguruma kama dubu na kuomboleza kama njiwa; tunasubiria haki, lakini hakuna kitu; kwa ukombozi, lakini uko mbali na sisi.
כי רבו פשעינו נגדך וחטאותינו ענתה בנו כי פשעינו אתנו ועונתינו ידענום 12
Maana makosa yetu mengi yako mbele zako, na dhambi zetu zinatushuhudia sisi; maana makosa yako pamoja na sisi.
פשע וכחש ביהוה ונסוג מאחר אלהינו דבר עשק וסרה הרו והגו מלב דברי שקר 13
Tumeaasi, kumkana Yahwe na kuacha kumfuata Mungu. Tulizungumzia ulafi kujeuka nyuma, na kuanza kulalamika kutoka moyoni na maneno ya uongo.
והסג אחור משפט וצדקה מרחוק תעמד כי כשלה ברחוב אמת ונכחה לא תוכל לבוא 14
Haki imerudishwa nyuma, wenye haki wamesimama mbali sana; maana ukweli uko mashakani katika mraba wa umma, haki haiwezi kuja.
ותהי האמת נעדרת וסר מרע משתולל וירא יהוה וירע בעיניו כי אין משפט 15
Waaminifu wamenda zao, na yeyote anayegeuka mbali na maovu anajiathiri mwenyewe. Yahwe aliliona hilo na hakupendezwa maana hakuna haki.
וירא כי אין איש וישתומם כי אין מפגיע ותושע לו זרעו וצדקתו היא סמכתהו 16
Aliona kwamba hakuna mtu, na akastaajabu kwamba hakuna mtu wa kuoma. Hivyo basi mkono wake uliletao wakovu kwake, na haki yake unamtosheleza yeye.
וילבש צדקה כשרין וכובע ישועה בראשו וילבש בגדי נקם תלבשת ויעט כמעיל קנאה 17
Huivaa haki kama ngao kifuani na kofia ya chuma ya wokovu kichwani mwake. Anajivika mwenyewe kwa mavazi ya kisasi na kuvaa vazi la bidii.
כעל גמלות כעל ישלם--חמה לצריו גמול לאיביו לאיים גמול ישלם 18
Analipa tena kwa kilichotokea, hukumu ya hasira kwa adui zake na kwa adui atairidisha adhabu ya kisiwa kama zawadi yao.
ויראו ממערב את שם יהוה וממזרח שמש את כבודו כי יבוא כנהר צר רוח יהוה נססה בו 19
Hivyo wataliogopa jina la Yahwe kutoka magharibi na utukufu wake kutoka mashariki; maana atakuja kama mkondo wa mto, inaendeshwa na pumzi ya Yahwe.
ובא לציון גואל ולשבי פשע ביעקב--נאם יהוה 20
Mkombozi atakuja Sayuni na wale watkaojeuka kutoka matendo yao ya uasi katika nyumba ya Yakobo- Hili ni tamko la Yahwe.
ואני זאת בריתי אותם אמר יהוה--רוחי אשר עליך ודברי אשר שמתי בפיך לא ימושו מפיך ומפי זרעך ומפי זרע זרעך אמר יהוה מעתה ועד עולם 21
Na kama mimi, hili ni agano langu pamoja nao- asema Yahwe- Roho yangu iliyo juu yenu, na maneno yangu niliyoyaweka kinywani mwenu, hayataondoka midomo mwenu au kuodoka mbali na midomo wajukuu wenu, au kwenda mbali asema Yahwe- kuanziia sasa na hata milele.''

< ישעה 59 >