< מיכה 5 >

עתה תתגדדי בת גדוד מצור שם עלינו בשבט יכו על הלחי את שפט ישראל 1
Sasa njoni pamoja katika safu ya kupigana, binti wa maaskari; maaskari wameuzingira mji, kwa ufito watampiga mwamuzi wa Israeli kwenye shavu.
ואתה בית לחם אפרתה צעיר להיות באלפי יהודה--ממך לי יצא להיות מושל בישראל ומוצאתיו מקדם מימי עולם 2
Lakini wewe, Bethlehemu Efrata, hata kama uko mdogo miongoni mwa koo za Yuda, kutoka kweko mmoja atakuja kwangu kutawala Israeli, ambaye mwanzo wake ni kutoka nyakati za kale, toka milele.
לכן יתנם עד עת יולדה ילדה ויתר אחיו ישובון על בני ישראל 3
Kwa hiyo Mungu atawapa, hata mda wa yeye aliye katika uchungu kuzaa mtoto, na mabaki ya ndugu zake yatawarudia wana wa Israeli.
ועמד ורעה בעז יהוה--בגאון שם יהוה אלהיו וישבו כי עתה יגדל עד אפסי ארץ 4
Atasimama na kuchunga kundi lake kwa nguvu za Yahwe, kwa ukuu wa enzi ya jina la Yahwe Mungu wake. Watabaki, kwa kuwa atakuwa mashuhuri hata mwisho wa dunia.
והיה זה שלום אשור כי יבוא בארצנו וכי ידרך בארמנותינו והקמנו עליו שבעה רעים ושמנה נסיכי אדם 5
Atakuwa amani yetu. Wakati Waashuru watakapokuja kwenye nchi yetu, wakati wakitembea dhidi ya boma yetu, kisha kisha tutainuka juu yao wachungaji saba na viongozi nane juu ya watu.
ורעו את ארץ אשור בחרב ואת ארץ נמרד בפתחיה והציל מאשור--כי יבוא בארצנו וכי ידרך בגבולנו 6
Watachunga nchi ya Ashuru kwa upanga, na nchi ya Nimrodi katika malango yake. Atatuokoa kutoka kwa Waashuru, watakapokuja kwenye nchi yetu, watakapoingia kwenye mipaka yetu.
והיה שארית יעקב בקרב עמים רבים כטל מאת יהוה כרביבים עלי עשב--אשר לא יקוה לאיש ולא ייחל לבני אדם 7
Mabaki ya Yakobo yatakuwa katika kabila za watu wengi, kama umande utokao kwa Yahwe, kama manyunyu kwenye majani, ambayo hayamsubiri mtu, na hayawasubiri watoto wa mwanadamu.
והיה שארית יעקב בגוים בקרב עמים רבים כאריה בבהמות יער ככפיר בעדרי צאן--אשר אם עבר ורמס וטרף ואין מציל 8
Mabaki ya Yakobo yatakuwa miongoni mwa mataifa, miongoni mwa watu wengi, kama simba katikati ya kundi la kondoo. wakati akipita katikati yao, atawakanyaga juu yao na kuwachachana kuwa vipande vipande, na hakutakuwa na mtu wa kuwaokoa.
תרם ידך על צריך וכל איביך יכרתו 9
Mkono wako utainuliwa dhidi ya maadui zako, na utawaharibu.
והיה ביום ההוא נאם יהוה והכרתי סוסיך מקרבך והאבדתי מרכבתיך 10
“Itatokea siku hiyo,” asema Yahwe, “kwamba nitawaharibu farasi wako kutoka miongoni mwenu na nitayavunja magari yako ya farasi.
והכרתי ערי ארצך והרסתי כל מבצריך 11
Nitaiharibu miji katika nchi yako na kuzingusha ngome zako zote.
והכרתי כשפים מידך ומעוננים לא יהיו לך 12
Nitauharibu uchawi kwenye mkono wako, na hakutakuwa na waaguzi tena.
והכרתי פסיליך ומצבותיך מקרבך ולא תשתחוה עוד למעשה ידיך 13
Nitaziaharibu sanamu zako za pango na nguzo za mawe kutoka miongoni mwako. Hautaabudu tena ustadi wa mikono yako.
ונתשתי אשיריך מקרבך והשמדתי עריך 14
Nitazin'goa nguzo zako za Ashera kutoka miongoni mwenu, na nitaiharibu miji yenu.
ועשיתי באף ובחמה נקם--את הגוים אשר לא שמעו 15
Nitalipiza kisasi kwa hasira na ghadhabu juu ya mataifa ambayo hayakusikiliza.”

< מיכה 5 >