< תהילים 65 >

למנצח מזמור לדוד שיר ב לך דמיה תהלה אלהים בציון ולך ישלם-נדר 1
Kwako wewe, Mungu katika Sayuni, sifa zetu za kungoja; viapo vyetu vitaletwa kwako.
שמע תפלה-- עדיך כל-בשר יבאו 2
Wewe usikiaye maombi yetu, miili yote itakuja kwako.
דברי עונת גברו מני פשעינו אתה תכפרם 3
Maovu yanatutawala sisi; kama yalivyo makosa yetu, wewe utayasamehe.
אשרי תבחר ותקרב-- ישכן חצריך נשבעה בטוב ביתך קדש היכלך 4
Amebarikiwa mtu yule ambaye wewe huchagua kumsogeza karibu yako ili kwamba aishi hekaluni mwako. Tutatoshelezwa kwa uzuri wa nyumba yako, hekalu lako takatifu.
נוראות בצדק תעננו-- אלהי ישענו מבטח כל-קצוי-ארץ וים רחקים 5
Katika haki wewe utatujibu sisi kwa kufanya mambo ya ajabu, Mungu wa wokovu wetu; wewe ambaye ni ujasiri wa mwisho wote wa nchi na wa wale walio mbali toka pande za bahari.
מכין הרים בכחו נאזר בגבורה 6
Kwa manaa ni wewe ndiye uliyeifanya milima imara, wewe ambaye umefungwa mkanda wa uweza.
משביח שאון ימים--שאון גליהם והמון לאמים 7
Ni wewe unyamazishaye ngurumo za baharini; ngurumo za mawimbi yake, na vurugu za watu.
וייראו ישבי קצות--מאותתיך מוצאי בקר וערב תרנין 8
Wale wanaoishi sehemu za mwisho kabisa wa nchi wanaogopa ushahidi wa matendo yako; wewe hufanya mashariki na magharibi kushangilia.
פקדת הארץ ותשקקה רבת תעשרנה-- פלג אלהים מלא מים תכין דגנם כי-כן תכינה 9
Wewe huja kuisaidia nchi; unainyeshea inchi; wewe unaiimarisha nchi vizuri; mto wa Mungu umejaa maji; wewe humpa mwanadamu nafaka unapokuwa umekwisha iandaa nchi.
תלמיה רוה נחת גדודה ברביבים תמגגנה צמחה תברך 10
Wewe huyajaza matuta maji ya kutosha; wapasawazisha palipoinuka; wailainisha nchi kwa manyunyu ya mvua; waibariki mimea kati yao.
עטרת שנת טובתך ומעגליך ירעפון דשן 11
Umeuvika mwaka taji ya wema wako; mvumo wa mapito yako hudondosha unono katika nchi.
ירעפו נאות מדבר וגיל גבעות תחגרנה 12
Majani ya nyikani hudondosha umande, na vilima vimevikwa furaha.
לבשו כרים הצאן-- ועמקים יעטפו-בר יתרועעו אף-ישירו 13
Malisho yamevishwa mifugo; mabonde pia yamefunikwa na nafaka; yanapiga kelele za shangwe, nayo yanaimba.

< תהילים 65 >