< 箴言 知恵の泉 11 >

1 偽りのはかりは主に憎まれ、正しいふんどうは彼に喜ばれる。
Yehova huchukia vipimo ambavyo havipo sahihi, bali hufurahia uzani dhahiri.
2 高ぶりが来れば、恥もまた来る、へりくだる者には知恵がある。
Kinapokuja kiburi, ndipo aibu huja, bali unyenyekevu huleta hekima.
3 正しい者の誠実はその人を導き、不信実な者のよこしまはその人を滅ぼす。
Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali udanganyifu wa njia za wajanja utawaangamiza.
4 宝は怒りの日に益なく、正義は人を救い出して、死を免れさせる。
Utajiri hauna thamani siku ya ghadhabu, bali kwa kutenda haki hujilinda na mauti.
5 誠実な者は、その正義によって、その道をまっすぐにせられ、悪しき者は、その悪によって倒れる。
Mwenendo wa mtu mwema huinyosha njia yake, bali waovu wataanguka kwa sababu ya uovu wao.
6 正しい者はその正義によって救われ、不信実な者は自分の欲によって捕えられる。
Mwenendo mwema wa wale wampendezao Mungu utawalinda salama, bali wadanganyifu hunaswa katika shauku zao.
7 悪しき者は死ぬとき、その望みは絶え、不信心な者の望みもまた絶える。
Mtu mwovu anapokufa, tumaini lake hupotea na tumaini lililokuwa katika nguvu zake linakuwa si kitu.
8 正しい者は、悩みから救われ、悪しき者は代ってそれに陥る。
Yule atendaye haki hulindwa katika taabu na badala yake taabu humjia mwovu.
9 不信心な者はその口をもって隣り人を滅ぼす、正しい者は知識によって救われる。
Kwa kinywa chake asiyeamini Mungu humwangamiza jirani yake, bali kwa maarifa wale watendao haki hulindwa salama.
10 正しい者が、しあわせになれば、その町は喜び、悪しき者が滅びると、喜びの声がおこる。
Wanapofanikiwa watendao haki, mji hufurahi, waovu wanapoangamia, kunakuwa na kelele za furaha.
11 町は正しい者の祝福によって、高くあげられ、悪しき者の口によって、滅ぼされる。
Kwa zawadi nzuri za wale wanaompendeza Mungu, mji unakuwa mkubwa; kwa kinywa cha waovu mji huvurugwa.
12 隣り人を侮る者は知恵がない、さとき人は口をつぐむ。
Mtu mwenye dharau kwa rafiki yake hana akili, bali mtu mwenye ufahamu hunyamaza.
13 人のよしあしを言いあるく者は秘密をもらす、心の忠信なる者は事を隠す。
Anayekwenda akizunguka kwa kukashifu hufunua siri, bali mtu mwaminifu hustiri jambo.
14 指導者がなければ民は倒れ、助言者が多ければ安全である。
Pasipokuwa na uongozi wenye busara, taifa huanguka, bali ushindi huja kwa kushauriana washauri wengi.
15 他人のために保証をする者は苦しみをうけ、保証をきらう者は安全である。
Anayemdhamini mkopo wa mgeni ataumia kwa usumbufu, bali anayechukia kutoa rehani kwa namna ya ahadi yupo salama.
16 しとやかな女は、誉を得、強暴な男は富を得る。
Mwanamke mwenye rehema hupata heshima, bali watu wakorofi hufumbata utajiri.
17 いつくしみある者はおのれ自身に益を得、残忍な者はおのれの身をそこなう。
Mtu mkarimu hufaidika mwenyewe, bali mkatili hujiumiza mwenyewe.
18 悪しき者の得る報いはむなしく、正義を播く者は確かな報いを得る。
Mtu mwovu husema uongo kupata mishahara yake, bali yeye apandaye haki anavuna mishahara ya kweli.
19 正義を堅く保つ者は命に至り、悪を追い求める者は死を招く。
Mtu mwaminifu atendaye haki ataishi, bali yeye atendaye uovu atakufa.
20 心のねじけた者は主に憎まれ、まっすぐに道を歩む者は彼に喜ばれる。
Yehova anawachukia wenye ukaidi mioyoni, bali anawapenda wale ambao njia zao hazina makosa.
21 確かに、悪人は罰を免れない、しかし正しい人は救を得る。
Uwe na uhakika juu ya hili- watu waovu hawatakosa adhabu, bali uzao wa wale watendao haki watawekwa salama.
22 美しい女の慎みがないのは、金の輪の、ぶたの鼻にあるようだ。
Kama pete ya dhahabu kwenye pua ya nguruwe ndiyo alivyo mwanamke mzuri asiye na busara.
23 正しい者の願いは、すべて良い結果を得、悪しき者の望みは怒りに至る。
Shauku ya wale watendao haki ni matokeo mema, bali watu waovu wanaweza kutumainia ghadhabu tu.
24 施し散らして、なお富を増す人があり、与えるべきものを惜しんで、かえって貧しくなる者がある。
Kuna yule ambaye hupanda mbegu- atakusanya zaidi; mwingine hapandi- huyo anakuwa masikini.
25 物惜しみしない者は富み、人を潤す者は自分も潤される。
Mtu mkarimu atafanikiwa na yule awapaye maji wengine atapata maji yake mwenyewe.
26 穀物を、しまい込んで売らない者は民にのろわれる、それを売る者のこうべには祝福がある。
Watu wanamlaani mtu ambaye hukataa kuuza nafaka, bali zawadi njema hufunika kichwa chake ambaye huuza nafaka.
27 善を求める者は恵みを得る、悪を求める者には悪が来る。
Yule ambaye hutafuta mema kwa bidii pia anatafuta kibali, bali yule atafutaye ubaya atapata ubaya.
28 自分の富を頼む者は衰える、正しい者は木の青葉のように栄える。
Wale wanaotumaini utajiri wataanguka, bali kama jani, wale watendao haki watasitawi.
29 自分の家族を苦しめる者は風を所有とする、愚かな者は心のさとき者のしもべとなる。
Yule ambaye analeta taabu kwenye kaya yake ataurithi upepo na mpumbavu atakuwa mtumishi wa wenye moyo wa hekima.
30 正しい者の結ぶ実は命の木である、不法な者は人の命をとる。
Wale watendao haki watakuwa kama mti wa uzima, lakini vurugu huondoa uzima.
31 もし正しい者がこの世で罰せられるならば、悪しき者と罪びととは、なおさらである。
Tazama! Ikiwa wale watendao haki hupokea wanachositahili, je si zaidi kwa waovu na wenye dhambi!

< 箴言 知恵の泉 11 >