< Lucam 12 >

1 multis autem turbis circumstantibus ita ut se invicem conculcarent coepit dicere ad discipulos suos adtendite a fermento Pharisaeorum quae est hypocrisis
Kwa wakati huo, maelfu mengi ya watu walikusanyika pamoja, kiasi cha kuanza kukanyagana, akaanza kusema na wanafunzi wake kwanza, “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo ambayo ni unafiki”
2 nihil autem opertum est quod non reveletur neque absconditum quod non sciatur
Na hapatakuwepo na siri iliyofichika ambayo haitafunuliwa, wala jambo lililofichwa ambalo halitajulikana.
3 quoniam quae in tenebris dixistis in lumine dicentur et quod in aurem locuti estis in cubiculis praedicabitur in tectis
Na lolote mlilolisema katika giza, litasikiwa katika mwanga. Na yoyote mliyoyasema kwenye sikio ndani ya vyumba vyenu vya ndani vilivyofungwa yatatangazwa juu ya paa la nyumba.
4 dico autem vobis amicis meis ne terreamini ab his qui occidunt corpus et post haec non habent amplius quod faciant
Nawaambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili na kisha hawana kitu kingine cha kufanya,
5 ostendam autem vobis quem timeatis timete eum qui postquam occiderit habet potestatem mittere in gehennam ita dico vobis hunc timete (Geenna g1067)
Lakini nitawaonya mtakaye mwogopa. Mwogopeni yule ambaye baada ya kuwa ameua, ana mamlaka ya kutupa jehanamu. Ndiyo, nawaambiani ninyi, mwogopeni huyo. (Geenna g1067)
6 nonne quinque passeres veneunt dipundio et unus ex illis non est in oblivione coram Deo
Je shomoro watano hawauzwi kwa sarafu mbili? hata hivyo hakuna hata mmoja wao atakayesahaulika mbele za Mungu.
7 sed et capilli capitis vestri omnes numerati sunt nolite ergo timere multis passeribus pluris estis
Lakini mjue kuwa, nywele za vichwa vyenu vimehesabiwa. Msiogope. Ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi.
8 dico autem vobis omnis quicumque confessus fuerit in me coram hominibus et Filius hominis confitebitur in illo coram angelis Dei
Ninawaambia, yeyote atakayenikiri Mimi mbele za watu, Mwana wa Adamu atamkiri mbele za malaika wa Mungu.
9 qui autem negaverit me coram hominibus denegabitur coram angelis Dei
Lakini yeyeyote atakayenikana mbele za watu naye atakanwa mbele ya Malaika wa Mungu.
10 et omnis qui dicit verbum in Filium hominis remittetur illi ei autem qui in Spiritum Sanctum blasphemaverit non remittetur
Yeyote atakayesema neno baya juu ya Mwana wa Adamu, atasamehewa, lakini yeyote atakayemkufuru Roho Mtakatifu, hatasamehewa.
11 cum autem inducent vos in synagogas et ad magistratus et potestates nolite solliciti esse qualiter aut quid respondeatis aut quid dicatis
Watakapowapeleka mbele za wakuu wa masinagogi, watawala, na wanye mamlaka, msiogope juu na namna ya kuongea katika kujitetea au nini mtakachosema,
12 Spiritus enim Sanctus docebit vos in ipsa hora quae oporteat dicere
kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha namna mtakavyosema kwa wakati huo.”
13 ait autem quidam ei de turba magister dic fratri meo ut dividat mecum hereditatem
Mtu mmoja katika kusanyiko akamwambia, “Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie sehemu ya uruthi wangu.”
14 at ille dixit ei homo quis me constituit iudicem aut divisorem super vos
Yesu akamjibu, ni nani aliye niweka kuwa mwamuzi na mpatanishi kati yenu?
15 dixitque ad illos videte et cavete ab omni avaritia quia non in abundantia cuiusquam vita eius est ex his quae possidet
Ndipo akawaambia, Jihadharini na kila namna ya tamaa, kwa sababu uzima wa mtu hauko katika wingi wa vitu alivyo navyo.”
16 dixit autem similitudinem ad illos dicens hominis cuiusdam divitis uberes fructus ager adtulit
Yesu akawaambia mfano, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilizaa sana,
17 et cogitabat intra se dicens quid faciam quod non habeo quo congregem fructus meos
na akajiuliza ndani yake, akisema, nitafanyaje kwani sina mahali pa kuhifadhi mazao yangu?
18 et dixit hoc faciam destruam horrea mea et maiora faciam et illuc congregabo omnia quae nata sunt mihi et bona mea
Akasema, nitafanya hivi. Nitavunja ghala zangu ndogo na kujenga iliyo kubwa, na kuyahifadhi mazao yangu yote na vitu vingine.
19 et dicam animae meae anima habes multa bona posita in annos plurimos requiesce comede bibe epulare
Nitaiambia nafsi yangu, “Nafsi, umejiwekea akiba ya vitu vingi kwa miaka mingi. Pumzika, ule, unywe na kustarehe.”
20 dixit autem illi Deus stulte hac nocte animam tuam repetunt a te quae autem parasti cuius erunt
Lakini Mungu akamwambia, ewe mtu mpumbavu, usiku wa leo wanahitaji roho kutoka kwako, na vitu vyote ulivyoviandaa vitakuwa vya nini?
21 sic est qui sibi thesaurizat et non est in Deum dives
Ndivyo itakavyokuwa kwa kila mtu anayejiwekea mali na si kujitajirisha kwa ajili ya Bwana.
22 dixitque ad discipulos suos ideo dico vobis nolite solliciti esse animae quid manducetis neque corpori quid vestiamini
Yesu akawaambia wanafunzi wake, Kwa hiyo nawaambia msihofu juu ya maisha yenu ya kuwa mtakula nini au juu ya miili yenu ya kuwa mtavaa nini
23 anima plus est quam esca et corpus quam vestimentum
Kwa kuwa maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi.
24 considerate corvos quia non seminant neque metunt quibus non est cellarium neque horreum et Deus pascit illos quanto magis vos pluris estis illis
Angalieni ndege wa angani, hawalimi wala hawavuni. Hawana chumba wala ghala ya kuhifadhia, lakini Baba yenu huwalisha. Ninyi si bora zaidi kuliko ndege!
25 quis autem vestrum cogitando potest adicere ad staturam suam cubitum unum
Ni yupi kati yenu ambaye akijisumbua ataweza kuongeza dhiraa moja katika maisha yake?
26 si ergo neque quod minimum est potestis quid de ceteris solliciti estis
Ikiwa basi hamuwezi kufanya hicho kitu kidogo kilicho rahisi kwa nini basi kusumbukia hayo mengine?
27 considerate lilia quomodo crescunt non laborant non nent dico autem vobis nec Salomon in omni gloria sua vestiebatur sicut unum ex istis
Angalieni maua -yanavyomea. Hayafanyi kazi wala hayasokoti. Lakini nawaambia, hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama mojawapo ya haya,
28 si autem faenum quod hodie in agro est et cras in clibanum mittitur Deus sic vestit quanto magis vos pusillae fidei
Kama Mungu huyavika vizuri majani ya kondeni, ambayo leo yapo, na kesho hutupwa kwenye moto. Je si zaidi atawavika ninyi? enyi wa imani haba!
29 et vos nolite quaerere quid manducetis aut quid bibatis et nolite in sublime tolli
Msisumbukie juu ya kuwa mtakula nini au mtakunywa nini, wala msiwe na hofu.
30 haec enim omnia gentes mundi quaerunt Pater autem vester scit quoniam his indigetis
Kwa kuwa Mataifa yote ya dunia husumbukia mambao yao. Na Baba yenu anajua ya kuwa mnahitaji hayo.
31 verumtamen quaerite regnum Dei et haec omnia adicientur vobis
Lakini tafuteni ufalme wake kwanza, na hayo mengine mtazidishiwa,
32 nolite timere pusillus grex quia conplacuit Patri vestro dare vobis regnum
msiogope, enyi kundi dogo, kwa sababu Baba yenu anafurahia kuwapa ninyi huo ufalme.
33 vendite quae possidetis et date elemosynam facite vobis sacculos qui non veterescunt thesaurum non deficientem in caelis quo fur non adpropiat neque tinea corrumpit
Uzeni mali zenu na mkawape maskini, mjifanyie mifuko isiyoishiwa hazina ya mbinguni isiyokoma, sehemu ambapo wezi hawatakaribia wala nondo haitaweza kuharibu.
34 ubi enim thesaurus vester est ibi et cor vestrum erit
Kwa kuwa palipo na hazina yako, ndipo na roho yako itakapokuwepo.
35 sint lumbi vestri praecincti et lucernae ardentes
Nguo zenu ndefu ziwe zimefungwa kwa mkanda, na taa zenu zihakikishwe kuwa zinaendelee kuwaka,
36 et vos similes hominibus expectantibus dominum suum quando revertatur a nuptiis ut cum venerit et pulsaverit confestim aperiant ei
na muwe kama watu wanaomtazamia Bwana wao kutoka kwenye sherehe ya harusi, ili kwamba akija na kupiga hodi, wataweze kumfungulia mlango kwa haraka.
37 beati servi illi quos cum venerit dominus invenerit vigilantes amen dico vobis quod praecinget se et faciet illos discumbere et transiens ministrabit illis
Wamebarikiwa wale watumishi, ambao Bwana atawakuta wako macho. Hakika atafunga nguo yake ndefu kwa mkanda, kisha atawaketisha chini kwa chakula, na kisha kuwahudumia.
38 et si venerit in secunda vigilia et si in tertia vigilia venerit et ita invenerit beati sunt servi illi
Kama Bwana atakuja kwa zamu ya pili ya ulinzi ya usiku, au hata zamu ya tatu ya ulinzi, na kuwakuta wakiwa tayari, itakuwa ni heri kwa hao watumishi.
39 hoc autem scitote quia si sciret pater familias qua hora fur veniret vigilaret utique et non sineret perfodiri domum suam
Zaidi ya hayo, mjue hili, kama bwana mwenye nyumba angelijua saa ambayo mwivi anakuja, asingeliruhusu nyumba yake ifunjwe.
40 et vos estote parati quia qua hora non putatis Filius hominis venit
Iweni tayari pia kwani hamjui ni wakati gani mwana wa Adamu atarudi.
41 ait autem ei Petrus Domine ad nos dicis hanc parabolam an et ad omnes
Petro akasema, “Bwana, watuambia sisi wenyewe hii mifano, au unamwambia kila mtu?
42 dixit autem Dominus quis putas est fidelis dispensator et prudens quem constituet dominus super familiam suam ut det illis in tempore tritici mensuram
Bwana akawaambia, “Ni nani mtumwa mwaminifu au mwenye hekima ambaye bwana wake atamweka juu ya watumishi wengine, ili awagawie chakula chao kwa wakati mwafaka?
43 beatus ille servus quem cum venerit dominus invenerit ita facientem
Amebarikiwa mtumishi yule, ambaye bwana wake akija atamkuta akifanya yale aliyoagizwa.
44 vere dico vobis quia supra omnia quae possidet constituet illum
Hakika nawaambia ninyi ya kuwa atamweka juu ya mali yake yote.
45 quod si dixerit servus ille in corde suo moram facit dominus meus venire et coeperit percutere pueros et ancillas et edere et bibere et inebriari
Lakini Mtumishi yule akisema moyoni mwake, “bwana wangu anachelewa kurudi; hivyo akaanza kuwapiga wale watumishi wa kiume na wa kike, kisha akaanza kula, kunywa na kulewa,
46 veniet dominus servi illius in die qua non sperat et hora qua nescit et dividet eum partemque eius cum infidelibus ponet
bwana wake yule mtumwa atakuja katika siku asiyotegemea na saa asiyoijua, naye atamkata vipande vipande na kumuweka katika sehemu pamoja na wasiokuwawaaminifu'
47 ille autem servus qui cognovit voluntatem domini sui et non praeparavit et non fecit secundum voluntatem eius vapulabit multas
Mtumishi, anayejua mapenzi ya bwana wake, naye hakujiandaaa wala hakufanya sawa sawa na mapenzi yake, atapigwa viboko vingi.
48 qui autem non cognovit et fecit digna plagis vapulabit paucis omni autem cui multum datum est multum quaeretur ab eo et cui commendaverunt multum plus petent ab eo
Lakini mtumishi asiyejua mapenzi ya bwana wake, lakini akafanya yanayostahili adhabu, atapigwa viboko vichache. Kwa kuwa yeye aliyepewa vingi, vingi hudaiwa kutoka kwake, na yeye aliyeaminiwa kwa vingi, kwake vitadaiwa vingi zaidi.
49 ignem veni mittere in terram et quid volo si accendatur
Nimekuja kuwasha moto duniani, na natamani iwe umekwishawaka,
50 baptisma autem habeo baptizari et quomodo coartor usque dum perficiatur
Lakini nina ubatizo ambao nitabatizwa, na nina huzuni mpaka utkapokamilika!
51 putatis quia pacem veni dare in terram non dico vobis sed separationem
Je mnafikiri kuwa nimekuja kuleta amani duniani? Hapana, Nawaambieni, badala yake nimeleta mgawanyiko.
52 erunt enim ex hoc quinque in domo una divisi tres in duo et duo in tres
Tangu sasa na kuendelea kutakuwa na watu watano katika nyumba moja wamegawanyika, na watatu watakuwa kinyume na wawili, na wawili watakuwa kinyume na watatu.
53 dividentur pater in filium et filius in patrem suum mater in filiam et filia in matrem socrus in nurum suam et nurus in socrum suam
Watagawanyika, baba atakuwa kinyume na mwanae, na mwanae atakuwa kinyume na babaye, mama atakuwa kinyume na binti yake, na binti atakuwa kinyume na mama yake, Mama mkwe atakuwa kinyume na mkwe wake naye mkwe atakuwa kinyume na mama mkwe wake.
54 dicebat autem et ad turbas cum videritis nubem orientem ab occasu statim dicitis nimbus venit et ita fit
Yesu akawa anawaambia makutano pia, “Mara muonapo mawingu yakitokea magharibi, mnasema nyakati za mvua zimewadia; na ndivyo inavyo kuwa,
55 et cum austrum flantem dicitis quia aestus erit et fit
Na upepo wa kusini ukivuma, mnasema, Patakuwepo na joto kali, na ndivyo inavyokuwa.
56 hypocritae faciem terrae et caeli nostis probare hoc autem tempus quomodo non probatis
Enyi wanafiki, mnaweza kutafsiri mwonekano wa nchi na anga, lakini inakuwaje hamuwezi kuutafsiri wakati uliopo?
57 quid autem et a vobis ipsis non iudicatis quod iustum est
Ni kwa nini kila mmoja wenu asipambanue lililo sahihi kwake kulifanya wakati ambapo angali na nafasi ya kufanya hivyo?
58 cum autem vadis cum adversario tuo ad principem in via da operam liberari ab illo ne forte trahat te apud iudicem et iudex tradat te exactori et exactor mittat te in carcerem
Maana mkienda na mshitaki wako mbele ya hakimu, jitahidi kupatana na mshitaki wako mungali bado mko njiani asije akakupeleka kwa hakimu, na hakimu akupeleka kwa ofisa, na ofisa akakutupa gerezani.
59 dico tibi non exies inde donec etiam novissimum minutum reddas
Nakuambia, hutatoka huko hadi umelipa mpaka senti ya mwisho.

< Lucam 12 >