< Matendo ga Mitume 1 >

1 Kitabu cha kwaembo nikiandikie, Thefili, kanibaya goti Yesu atumbwi kugapanga na pundisha,
Kitabu cha zamani nilikiandika, Theofilo, nikisema yote Yesu aliyoanza kufanya na kufundisha,
2 mpaka lisoba ambayo ywembe atipokelewa kunani. Ayee yabile payapitike amri pitya kwa Roho mtakatifu kwa mitume bayomwile kuwachawaa.
mpaka siku ambayo Yeye alipokelewa juu. Hii ilikuwa baada ya kutoa amri kupitia Roho Mtakatifu kwa mitume aliokuwa amewachagua.
3 Baada ya teswa kwake, Jwembe abonekine panga aikoti nathibitika kwanansima kaishuhudia. Kwa masoba arobaini abonekine kasabe na alongela likowe lya Nnongo.
Baada ya mateso yake, Yeye alionekana kwao akiwa hai pia na vithibitisho vingi vikishuhudia. Kwa siku arobaini alijidhihirisha kwao, na alizungumza kuhusu ufalme wa Mungu.
4 Napabakwembine nabo pamope nabo, abakiye kana babuke Yerusalemu, ila balende kwa ajili ya ahadi ya Tate, bembe, batibaya, “Mwayowine boka kwango
Alipokuwa akikutana pamoja nao, aliwaamuru wasiondoke Yerusalemu, lakini wasubiri kwa ajili ya ahadi ya Baba, ambayo, alisema, “Mlisikia kutoka kwangu
5 panga Yohana alibatiza kabisa kwa mase, lakini ywabatizwa kwa Roho Mtakatifu katika masoba aga machunu.”
kwamba Yohana alibatiza kabisa kwa maji, lakini mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu katika siku hizi chache.”
6 Napabakwembine pamope batikwinaluya, “Ngwana muda go ngawa kelebukeya Israel ufalme?”
Na walipokuwa wamekutanika pamoja walimuuliza, “Bwana, hivi huu ndio muda utakaowarudishia Israeli ufalme?”
7 Jwembe atikwabakia, lyengo lino mwangali tanga majira ambayo Tate atikusudia kwa mamlaka gake mwene.”
Yeye akawaambia, “Siyo sawa kwenu kujua wakati au majira ambayo Baba amekusudia kwa mamlaka yake mwenyewe.”
8 Lakini mwapokya ngupu, wakati walowa icha Roho Mtakatifu kunani yinu na mwenga mwalowa panga masaidi bango mwabote mu'Yerusalemu na Uyahudi yoti na Samalia mpaka mwiso wa nchi.”
Lakini mtapokea nguvu, wakati Roho Mtakatifu atakapokuja juu yenu, na ninyi mtakuwa mashahidi wangu kote katika Yerusalemu na Uyahudi yote na Samaria mpaka mwisho wa nchi.”
9 Ngwana Yesu payomwile longela goo, pababile kabalolekeya kunani, ywembe apotwilile nnani, na liunde lyatikumwekelya bamweni likae kwa minyo gabe.
Bwana Yesu alipokwisha yasema haya, wakiwa wanatazama juu, Yeye aliinuliwa juu, na wingu likamfunika wasimwone kwa macho yao.
10 Wakati kabalolekeya kunani kayenda gapula, Bandu abele bayemi pakatikati yabe baweti mangobo mauu.
Wakati wanatazama mbinguni kwa makini akienda, ghafla, watu wawili walisimama katikati yao wamevaa mavazi meupe.
11 Batibaya, “Mwenga mwabandu ba Galilaya, mwanja namani muyema pa kumlolekeya kumaunde?” Ayoo Yesu ywangulwike kunani, alowa buyangana nyonyo kati mwamumweni kayenda kunani.
Walisema, “Enyi watu wa Galilaya, kwa nini mnasimama hapa mkitazama mbinguni?” Huyu Yesu aliyepaa juu mbinguni atarudi kwa namna ile ile kama mlivyomuona akienda mbinguni.
12 Ngababuyangana Yerusalemu boka pa kitombe sa Mizeituni, ambao ubile papipi ni Yerusalemu, mwendo wa lisoba lya Sabato.
Ndipo wakarudi Yerusalemu kutoka kwenye mlima wa mizeituni, ambao uko karibu na Yerusalemu, mwendo wa siku ya Sabato.
13 Pabaikite bayei mughorofa mwabatamage. Na bembe ni Petro, Yohana, Yakobo, Andrea, Filipo, Thomaso, Batholomayo, Mathayo, Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni Zelote na Yuda mwana wa Yakobo.
Walipofika walikwenda ghorofani walikokuwa wakikaa. Nao ni Petro, Yohana, Yakobo, Andrea, Filipo, Thomaso, Batholomayo, Mathayo, Yakobo Mwana wa Alfayo, Simoni Zelote na Yuda Mwana wa Yakobo.
14 Boti babile mpamo kati mundu yumo, kwa juhudi babile batiyendelya katika maombi pamope na ago babile anwawa, Mariamu mao gake Yesu, na anja bake.
Wote waliungana kama mtu mmoja, kwa juhudi walikuwa wakiendelea katika maombi. Pamoja na hao walikuwepo wanawake, Mariamu Mama yake Yesu, na kaka zake.
15 Katika masoba ago Petro ayemi katikati ya alongo, kati bandu 120, abaya,
Katika siku zile Petro alisimama katikati ya ndugu, kama watu 120, akasema,
16 Alongo, ibile lazima panga maandiko gatimizwe, ambapo zamani Roho Mtakatifu abaya kwa nkanwa wa Daudi husiana na Yuda, ambaye abaelekeza balo bankamwile Yesu.
Ndugu, ilikuwa lazima kwamba maandiko yatimizwe, ambapo zamani Roho Mtakatifu alisema kwa kinywa cha Daudi kuhusiana na Yuda, ambaye aliwaelekeza wale waliomkamata Yesu.
17 Mana ywembe abile yumo witu na apeyilwe lifungu lyake na faida ya ayee huduma.”
Kwa kuwa yeye alikuwa mmoja wetu na alipokea fungu lake la faida katika hii huduma.”
18 (Nambeambe yoo apemite lieneo kichelo chapeyilwe kwa ubaya wake atitumbuka alongwiye ntwee, yega yatipapwanika matumbu panja gatipekanika.
(Sasa mtu huyu alinunua eneo kwa kile alichokipokea kwa uovu wake na hapo alianguka akitanguliza kichwa, mwili ukapasuka na matumbo yake yote yakawa wazi yakamwagika.
19 Bote babatamaye Yerusalemu bayowine kuhusu likowe lee, na lieneo lyoo balikemite kwa lugha yabe “Akeldama” ango ni “ngunda wa myai.”)
Wote walioishi Yerusalemu walisikia kuhusu hili, hivyo eneo hilo wakaliita kwa lugha yao “Akeldama” hilo ni “shamba la damu.”)
20 “Mu kitabu sa Zaburi iandikilwe,” Lenda lenda lieneo lyake ube hame na kana iruhusiwe hata yumo tama palo,'na 'Ruhusa mundu ywenge aitole nafasi ya utawala.'
“Kwenye kitabu cha Zaburi imeandikwa, 'Ngoja eneo lake liwe hame na isiruhusiwe hata mmoja kuishi pale;' na, 'Ruhusu mtu mwingine achukue nafasi yake ya uongozi.'
21 Ayoo nga muhimu, kwa eyo, yumo wa alalome ambao batiambatana natwenga wakati Ngwana Yesu aboi na kujingya kati yitu,
Hiyo ni muhimu, kwa hiyo, mmoja wa wanaume ambao waliambatana nasi wakati Bwana Yesu alipotoka na kuingia kati yetu,
22 tumbwile mu'ubatizo wa Yohana mpaka lisoba lelo lyapotwilwe kunani, lazima abe shahidi ba ufunuo pamope ni twenga.
kuanzia kwenye ubatizo wa Yohana mpaka siku ile alipotwaliwa juu, lazima awe shahidi wa ufufuo pamoja nasi.
23 “Babekite nnongi yabe analome abele, Yusufu ywakemelwa Barnaba, ambae ywakemelwa Yusto na Mathia.
“Wakaweka mbele wanaume wawili, Yusufu aitwaye Barnaba, ambaye pia aliitwa Yusto na Mathia.
24 Bembe balobite kababaya, “Wenga, Ngwana, uitangite mioyo ya bandu bote, nga nyoo beka mbolika ywaako kati ya abele aba abachawile
Wao waliomba wakisema, “Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, hivyo weka wazi yupi kati ya wawili hawa ambaye umemchagua
25 kuitola nafasi katika huduma na utume, ambayo Yuda apangite ubou na yendya mahali pake.”
kuchukua nafasi katika huduma na utume, ambapo Yuda alitenda uovu na kwenda mahali pake.”
26 Bapigite kura kwa ajili yabe, na kura yatimwangukia Mathia ywabile atibalangilwa pamope na balo mitume komi na jimo.
Wakapiga kura kwa ajili yao, na kura ikamwangukia Mathia ambaye alihesabiwa pamoja na wale mitume kumi na moja.

< Matendo ga Mitume 1 >