< Akolosai 3 >

1 Mana itei kae Nnongo atikuwafufua pamope ni Kristo, mugapale makowe ya kunani ambako Kristo atama luboko lwa mmaliyo lwa Nnongo.
Basi, kwa kuwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo alikoketi mkono wa kuume wa Mungu.
2 Muwase kuhusu makowe ga kunani kuhusu kwaa makowe ga dunia.
Yafikirini mambo yaliyo juu, wala si ya duniani.
3 Kwa kuwa mwatiwaa, ni maisha yinu yayowanike kwaa pamope ni Kristo mu'Nnongo.
Kwa maana ninyi mlikufa, nao uhai wenu sasa umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.
4 Palyo Kristo alowa bonekana, ambae nga maisha yinu, nga mwenga kae mwalowa binekana niywembe mu'utukufu.
Wakati Kristo, aliye uzima wenu, atakapotokea, ndipo nanyi mtakapotokea pamoja naye katika utukufu.
5 Kwa eyo mugafikishe makowe galiyo mu'nnema yaani, umalaya, uchapu, shauku inoite kwaa, ni tamaa, ambayo nga ibada ya sanamu.
Kwa hiyo, ueni kabisa chochote kilicho ndani yenu cha asili ya kidunia: yaani uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya na ulafi, ambayo ndiyo ibada ya sanamu.
6 Ni kwaa ajili ya makowe aga gadhabu yaisa nnani ya bana babile kwaa nautii.
Kwa sababu ya mambo haya, ghadhabu ya Mungu inakuja.
7 Ni kwa ajili ya makowe aga mwenga kae mwatityanga kwake mwatamite nkati yabe.
Ninyi pia zamani mlienenda katika mambo haya mlipoishi maisha hayo.
8 Lakini nambeambe ni lazima mugaboye makowe aga gote. Yaani, gadhabu, hasira, nia inoite kwaa, matukangano, ni maneno machapu yaboka mu'mikano yinu.
Lakini sasa yawekeni mbali nanyi mambo kama haya yote: yaani hasira, ghadhabu, uovu, masingizio na lugha chafu kutoka midomoni mwenu.
9 Kana mubaye ubocho kati yinu mwenga, kwa mana mwatiuuluwa utu winu wa kinchogo ni makowe gake.
Msiambiane uongo, kwa maana mmevua kabisa utu wenu wa kale pamoja na matendo yake,
10 Mwatiuwala utu waayambe, ambao upangika wambeyambe mu'maarifa bokana ni mpwano wa yolo ywamuumbile.
nanyi mmevaa utu mpya, unaofanywa upya katika ufahamu sawasawa na mfano wa Muumba wake.
11 Mu'maarifa aga, ntopo myunani ni myahudi, tairiwa ni tairiwa kwaa, msomi, ywaabile kwaa msomi, mmanda, ni ywabile kwaa mmanda, lakini badala yake Kristo nga makowe goti nkati ya goti.
Hapa hakuna Myunani wala Myahudi, aliyetahiriwa wala asiyetahiriwa, asiyestaarabika wala aliyestaarabika, mtumwa wala mtu huru, bali Kristo ni yote, na ndani ya wote.
12 Kati bateule ba Nnongo, batakatifu ni apendwa, muuwale utu wema, ukarimu, unyenyekevu, upole ni uvumulivu.
Kwa hiyo, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
13 Muchukulyane mwenga kwa mwenga, Muhurumiane kila mundu ni mwenake. Kati mundu abile ni lilalamiko dhidi ya ywenge, amsamehe kwa namna yeyelo ambayo Ngwana atikuwa samiya mwenga.
Vumilianeni na kusameheana mtu akiwa na lalamiko lolote dhidi ya mwenzake. Sameheaneni kama vile Bwana alivyowasamehe ninyi.
14 Zaidi ya makowe aga goti, mube ni upendo ambao nga kigezo cha ukamilifu
Zaidi ya maadili haya yote jivikeni upendo, ambao ndio unaofunga kila kitu pamoja katika umoja mkamilifu.
15 Amani ya Kriso ni ibaongoze mu'mioyo yinu. Yabile ni kwa ajili ya amani yee kwamba mwati tiliwa mu'yega umo. Mube ni shukrani.
Amani ya Kristo na itawale mioyoni mwenu, kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena kuweni watu wa shukrani.
16 Na lineno lya Kristo litame nkati yinu kwa utajiri. Kwa hekima yoti, mupundishane ni kushauriana mwenga kwa mwenga kwa Zaburi, nyimbo, na nyimbo za mu'roho. Muimbe kwa shukrani mu'mioyo yinu kwa Nnongo.
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu.
17 Na chochote mukipangite, mu'maneno au mu'makowe, mupange yote mu'lina lya Ngwana Yesu. Mumpeye shukrani Nnongo tate pitya Ywembe.
Lolote mfanyalo, ikiwa ni kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba katika yeye.
18 Anwawa, muanyenyekee asengo binu, kati yatipendeza nkati ya Ngwana.
Ninyi wake, watiini waume zenu, kama inavyostahili katika Bwana.
19 Mwenga asengo, mwapende anyumbo yinu, na kana mube wakali dhidi yabe.
Ninyi waume, wapendeni wake zenu, wala msiwe na uchungu dhidi yao.
20 Bana, mubatii azazi winu mu'makowe yoti, mana nga impendeza Ngwana.
Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, kwa maana hivi ndivyo inavyompendeza Bwana.
21 Mwa tate kana muwachokoze bana binu, ili kwamba kana baise kata tamaa.
Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
22 Amanda, mubatii ngwana winu mu'yega kwa makowe yoti, kana ibe kwa huduma ya minyo kati bandu ba kupuraisha kae, ila kwa mwoyo wa kweli, Mun]yogope Nnongo.
Ninyi watumwa, watiini mabwana zenu wa hapa duniani katika mambo yote. Fanyeni hivyo si wakiwepo tu, wala si kwa kutafuta upendeleo wao, bali kwa moyo mnyofu na kumcha Bwana.
23 Chochote cha mukipanga, mupange kuoma mu'mwoyo winu kati Ngwana na kana ibe kati kwa bandu.
Lolote mfanyalo, fanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana, na si wanadamu,
24 Mutangite kuwa mwalowa pokya tuzo ya kumiliki kuoma kwa Ngwana. Ni Kristo Ngwana ywamwamumtumikya.
kwa kuwa mnajua kwamba mtapokea urithi wenu kutoka kwa Bwana ukiwa thawabu yenu. Ni Bwana Yesu Kristo mnayemtumikia.
25 Kwa sababu yeyote ywapanga yabile kwaa ga haki alowa pokya hukumu kwa matendo yabile kwaa haki yaipangite, ni ntopo upendeleo.
Yeyote atendaye mabaya atalipwa kwa ajili ya mabaya yake, wala hakuna upendeleo.

< Akolosai 3 >