< Maombolezo 5 >

1 Kumbuka, Ee Bwana, yaliyotupata, tazama, nawe uione aibu yetu.
זכר יהוה מה היה לנו הביט וראה את חרפתנו׃
2 Urithi wetu umegeuziwa kwa wageni, na nyumba zetu kwa wageni.
נחלתנו נהפכה לזרים בתינו לנכרים׃
3 Tumekuwa yatima wasio na baba, mama zetu wamekuwa kama wajane.
יתומים היינו אין אב אמתינו כאלמנות׃
4 Ni lazima tununue maji tunayokunywa, kuni zetu zapatikana tu kwa kununua.
מימינו בכסף שתינו עצינו במחיר יבאו׃
5 Wanaotufuatilia wapo kwenye visigino vyetu, tumechoka na hakuna pumziko.
על צוארנו נרדפנו יגענו לא הונח לנו׃
6 Tumejitolea kwa Misri na Ashuru tupate chakula cha kutosha.
מצרים נתנו יד אשור לשבע לחם׃
7 Baba zetu walitenda dhambi na hawapo tena, na sisi tunachukua adhabu yao.
אבתינו חטאו אינם אנחנו עונתיהם סבלנו׃
8 Watumwa wanatutawala na hakuna wa kutuokoa mikononi yao.
עבדים משלו בנו פרק אין מידם׃
9 Tunapata chakula chetu kwa kuhatarisha maisha yetu kwa sababu ya upanga jangwani.
בנפשנו נביא לחמנו מפני חרב המדבר׃
10 Ngozi yetu ina joto kama tanuru, kwa sababu ya fadhaa itokanayo na njaa.
עורנו כתנור נכמרו מפני זלעפות רעב׃
11 Wanawake wametendwa jeuri katika Sayuni, na mabikira katika miji ya Yuda.
נשים בציון ענו בתלת בערי יהודה׃
12 Wakuu wametungikwa juu kwa mikono yao, wazee hawapewi heshima.
שרים בידם נתלו פני זקנים לא נהדרו׃
13 Vijana wanataabika kwenye mawe ya kusagia, wavulana wanayumbayumba chini ya mizigo ya kuni.
בחורים טחון נשאו ונערים בעץ כשלו׃
14 Wazee wameondoka langoni la mji, vijana wameacha kuimba nyimbo zao.
זקנים משער שבתו בחורים מנגינתם׃
15 Furaha imeondoka mioyoni mwetu, kucheza kwetu kumegeuka maombolezo.
שבת משוש לבנו נהפך לאבל מחלנו׃
16 Taji imeanguka kutoka kichwani petu. Ole wetu, kwa maana tumetenda dhambi!
נפלה עטרת ראשנו אוי נא לנו כי חטאנו׃
17 Kwa sababu hiyo, mioyo yetu inazimia, kwa sababu ya hayo, macho yetu yamefifia,
על זה היה דוה לבנו על אלה חשכו עינינו׃
18 kwa ajili ya Mlima Sayuni, ambao unakaa ukiwa, nao mbweha wanatembea juu yake.
על הר ציון ששמם שועלים הלכו בו׃
19 Wewe, Ee Bwana unatawala milele, kiti chako cha enzi chadumu kizazi hadi kizazi.
אתה יהוה לעולם תשב כסאך לדר ודור׃
20 Kwa nini watusahau siku zote? Kwa nini umetuacha kwa muda mrefu?
למה לנצח תשכחנו תעזבנו לארך ימים׃
21 Turudishe kwako mwenyewe, Ee Bwana, ili tupate kurudi. Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale,
השיבנו יהוה אליך ונשוב חדש ימינו כקדם׃
22 isipokuwa uwe umetukataa kabisa na umetukasirikia pasipo kipimo.
כי אם מאס מאסתנו קצפת עלינו עד מאד׃

< Maombolezo 5 >