< 2 Wakorintho 7 >

1 Basi, wapenzi wangu, tukiwa tumepewa ahadi hizi zote, na tujitakase na chochote kiwezacho kuchafua miili na roho zetu, tuwe watakatifu kabisa, na tuishi kwa kumcha Mungu.
Having therefore these promises, beloved, let us cleanse ourselves from all defilement of flesh and spirit, perfecting holiness in the fear of God.
2 Tunaomba mtupe nafasi mioyoni mwenu! Hatujamkosea mtu yeyote, hatujamdhuru wala kumdanganya mtu yeyote.
Make room for us; we have wronged no one, we have corrupted no one, we have exploited no one.
3 Sisemi mambo haya kwa ajili ya kumhukumu mtu; maana, kama nilivyokwisha sema, ninyi mko mioyoni mwetu, tufe pamoja, tuishi pamoja.
I do not say this to condemn you; I have said before that you are in our hearts, whether to die together or to live together.
4 Nina imani kubwa sana ninaposema nanyi; naona fahari kubwa juu yenu! Katika taabu zetu nimepata kitulizo kikubwa na kufurahi mno.
I have great confidence in you; I do a lot of boasting about you. I am filled with encouragement, overflowing with joy in spite of all our affliction.
5 Hata baada ya kufika Makedonia hatukuweza kupumzika. Kila upande tulikabiliwa na taabu: nje ugomvi; ndani hofu.
Now indeed, when we came into Macedonia we had no physical rest, but were surrounded by affliction—conflicts on the outside, fears on the inside.
6 Lakini Mungu, mwenye kuwapa shime wanyonge alitupa moyo sisi pia kwa kuja kwake Tito.
But the God who encourages the lowly encouraged us by the coming of Titus;
7 Si tu kwa kule kuja kwake Tito, bali pia kwa sababu ya moyo mliompa ninyi. Yeye ametuarifu jinsi mnavyotamani kuniona, jinsi mlivyo na huzuni, na mnavyotaka kunitetea. Jambo hili linanifurahisha sana.
and not only by his coming, but also by how much he was encouraged over you as he reported to us your longing, your mourning, your zeal in my stead, so that I rejoiced even more.
8 Maana, hata kama kwa barua ile yangu nimewahuzunisha, sioni sababu ya kujuta. Naam, naona kwamba barua hiyo iliwatia huzuni lakini kwa muda.
Even though that letter caused you sorrow, I do not regret it (though I almost did), because I perceive that the letter made you sorry, though only for a while.
9 Sasa nafurahi, si kwa sababu mmehuzunika, ila kwa kuwa huzuni yenu imewafanya mbadili nia zenu na kutubu. Mmehuzunishwa kadiri ya mpango wa Mungu, na kwa sababu hiyo hatukuwadhuru ninyi kwa vyovyote.
Now I rejoice, not that you were made sorry, but that your sorrow led to repentance. For you were made sorry as God intended, so as not to be harmed by us in any way.
10 Kuwa na huzuni jinsi atakavyo Mungu, husababisha badiliko la moyo, badiliko lenye kuleta wokovu; hivyo hakuna sababu ya kujuta. Lakini huzuni ya kidunia huleta kifo.
Now godly sorrow produces repentance into salvation without regret, but the world's sorrow produces death.
11 Sasa mnaweza kuona matokeo ya kuona huzuni jinsi Mungu atakavyo: ninyi mmepata kuwa sasa watu wenye jitihada, wenye hoja, mnashtuka na kuogopa, mna bidii na mko tayari kuona kwamba haki yatekelezwa. Ninyi mmethibitisha kwa kila njia kwamba hamna hatia kuhusu jambo hili.
Just consider your own being caused to sorrow in a godly manner, how much diligence it produced in you—what self-defense, what indignation, what alarm, what longing, what zeal, what punishment! At every point you have demonstrated yourselves to be clear in the matter.
12 Hivyo, ingawa niliandika ile barua, haikuwa kwa ajili ya yule aliyekosa, au kwa ajili ya yule aliyekosewa. Niliandika kusudi ionekane wazi mbele ya Mungu jinsi mlivyo na bidii kwa ajili yetu.
So even though I wrote to you, it was not for the sake of the wrongdoer, nor for that of the victim, but, before God, so that your real commitment to us might be made clear to you.
13 Ndiyo maana sisi tulifarijika sana. Siyo kwamba tulifarijika tu, ila pia Tito alitufurahisha kwa furaha aliyokuwa nayo kutokana na jinsi mlivyomchangamsha moyo.
We have been encouraged by all this. Because of your encouragement, we rejoiced all the more over the joy of Titus, because his spirit has been refreshed by you all.
14 Mimi nimewasifu sana mbele yake, na katika jambo hilo sikudanganyika. Tumewaambieni ukweli daima, na kule kuwasifia ninyi mbele ya Tito kumekuwa jambo la ukweli mtupu.
Because wherein I boasted to him about you, I was not put to shame, but just as everything we spoke to you was true, so also our boasting to Titus proved to be true.
15 Hivyo upendo wake wa moyo kwenu unaongezeka zaidi akikumbuka jinsi ninyi nyote mlivyo tayari kutii, na jinsi mlivyomkaribisha kwa hofu nyingi na kutetemeka.
Also, his affection for you is all the greater, as he remembers your collective obedience as you received him with fear and trembling.
16 Nafurahi sana kwamba naweza kuwategemea ninyi kabisa katika kila jambo.
I am so glad that I have complete confidence in you.

< 2 Wakorintho 7 >